Hatukatai Wasanii wengi wanafanya muziki, wakati huo huo wanafanya biashara! Lakini kuna ushahidi wa wazi kabisa kwamba Wasanii wengi wanafanya biashara Kama extra work, yaana kazi ya ziada! Huku muziki ukiwa ndio kipaumbele Chao!!
👉Imekua Tofauti Kwa ndugu yetu billnas, yeye imekua kinyume chake yaaani biashara ndio ameitanguliza mbele ameacha muziki nyuma , sasa hapa lazima tu,atapotea kimuziki..
👉Huenda ,billnenga ameona muziki haumlipi😂 akaamua aanze kuuza simu ,
👉 Ukiangalia kwenye ukurasa wake wa Instagram billnas,kazi anayoifanya saizi nikutangaza tu simu zake ,amesahau kitu kilicho mfanya awe MAARUFU ,na afike pale ni muziki!
👉Hatukatai ,huwezi kufanya muziki milele lazima itafika kipindi utaacha tu ,lakini ifike wakati wakiona wenzao wanafanikiwa kimuziki wasilete wivu, waelewe kwamba wale wameikomalia kazi Yao inavyotakiwa , na wanaifanya Kwa moyo wote bila kuichanganya na mambo mengine, yaani hata kama wanafanya mambo mengine muziki wanaupa kipaumbele..
👉Billnass amebaki tu kulalamikaa nakutushauli "vijana tutafte pesaa, , mara "vijana tafteni pesa wanawake hawa hawaeleweki😂..ndugu yetu billnas anajua Kama Hana msimamo! Akomae na kitu kimoja bhnaa..
👉Tunamuona Nandy nae amekazana kumtangazia biashara ya simu ,billnas 😂huenda labda anahusika kwenye mtaji pale..yaaani inawezekanaje wawe kwenye migogoro ya mara Kwa mara,alafu akubali kumtangazia biashara ??lazima Nandy atakua amempa mtaji billnas..
👉 Kwahiyo huyu billnas ,tunashauri tu aache kuimba kwasababu inaonekana biashara anaiweza zaidi ,kuliko muziki , promotion anayoifanya kwenye biashara nikubwa kuliko aliokua anaifanya kwenye muziki..
👉Na mpaka sasa kuna watu,walishamsahau kabisa billnas, na ndomaana nimeunganisha na picha ya Nandy ili wamkumbuke vizuri.
By Sibongile
Post a Comment