Ali Kiba "Blue Ndio Alinipa Hamasa ya Kuingia Katika Muziki"






Alikiba alipata hamasa ya kuingia kwenye Bongofleva baada ya kuwaona Mr. Blue na Abby Skills wakitamba mwanzoni mwa miaka 2000s na baadaye walimsaidia pia ingawa Mr. Blue alimueka wazi mapema kuwa muziki sio masihara

“Nilipokuwa nikiwaangalia huku nikiwa tayari nina kauntabuku nyumbani limejaa mashairi na kati ya yake ulikuwamo wimbo wa Maria ambao niliwaandikia ili wauimbe (Mr Blue na Abby Skills)"

“Baada ya kuusikiliza, Blue alitaka na mimi niwe mmoja wa waimbaji katika wimbo huo na hapo ndio ukawa mwanzo wangu wa kutoboa mpaka mnavyoniona hii leo,” alisema Alikiba

Ikumbukwe Diamond pia alishasema alikuwa inspired na Mr. Blue alipomuona akifanya vizuri kwenye Bongo fleva akiwa na umri mdogo Mr. Blue, Diamond na Alikiba kiumri ni kama wapo rika moja Tu.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post