Zuma alazwa hospitalini kwa uangalizi wa kimatibabu




 
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelazwa katika hospitali nje ya gereza kwa ajili ya kufanyiwa uangalizi wa kimatibabu, wamesema maafisa wa gereza.

Wakfu wake umesema kuwa ulikuwa ni "uchunguzi wa kawaida wa kimatibabu wa kila mwaka" na kwamba "hakuna lolote la kutisha".

Kama rais wa zamani wa nchi, Zuma anatibiwa katika hospitali ya jeshi, maafisa wamesema.

Rais huyo wa zamani amekuwa akitumikia kifungo cha miezi 15 gerezani tangu alipohukumiwa tarehe 7 Julai kwa kutoheshimu agizo la mahakama.

Maafisa wa gereza wanasema kuwa ana haki ya kupata matibabu kama mfungwa mwingine yoyote yule anayefungwa gerezani.

Wizara ya sheria ilituma taarifa kamili kwenye mtandao wa Twitter.

Wiki ijayo, rais huyo wa zamani amepangiwa kufika mahakamani kwa tuhuma tofauti zinazohusiana na kesi ya ufisadi katika mkataba wa silaha.

Alikana mashitaka ya kuhusika katika mkataba huo wenye thamani ya dola bilioni 5 (£3bn).




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post