Zanzibar Wapiga Marufuku Mabweni Kuanzia Leo




KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali bwana Ali Khamis Juma amepiga marufuku kuwepo kwa dakhalia (MABWENI) za wanafunzi wa madarasa ya msingi kuanzia leo tarehe 15/8/2021 kwa Skuli zote za binafsi na Serikali.

Amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kukithiri vitendo vya Udhalilishaji katika dakhalia hizo na hivyo kuleta athari kubwa kwa jamii.

Akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na walimu wakuu wa Skuli za binafsi amesema vitendo vya udhakikishaji vimekuwa ni kero kwa jamii, hivyo ni vyema kushirikiana ili kupunguza au kuondoa kabisa vitendo hivyo.

Amefahamisha kuwa Wizara ya elimu inatarajia kuanzisha kitengo maalum cha Skuli binafsi kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili hivyo ni vyema kutoa ushirikiano ili kufanikisha suala hilo.


 
Amefahamisha kuwa mbali na kutoa changamoto pia ni kutoa fursa za kutoa ushauri kwa lengo la kuondoa matatizo na dhana mbaya kwa Skuli binafsi.

Amesema Skuli binafsi bado zina mchango mkubwa wa kutoa elimu kwa watoto kwa kuisaidia Serikali juu ya jukumu hilo, kama Serikali ilivyotoa ruhusu juu na kuzisajili skuli za binafsi kuendeleza elimu.

Nae Mkurugenzi Mipango sera na Utafiti Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali bw. Khalid Salum Waziri amesema mkutano huo una lengo la kuleta mabadiliko kati ya Skuli binafsi na wizara katika utoaji wa huduma bora za elimu.


Amesema kuna tatizo kwa baadhi ya Skuli za binafsi zinakataa kutoa usbirikiano katika masuala ya utoaji wa data hali ambayo inaleta tatizo wkati wanapopanga mipango yao katika kutoa huduma za kielimu katika skuli.

Amewataka kubadilika juu ya suala hilo kwani linasababisha ufanisi mdogo wakati wanapotaka kutoa huduma za kielimu katika Skuli.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Bi Asya Iddi Issa amewataka Walimu wakuu hao wa Skuli za binafsi kutowafukuza Skuli Wanafunzi kwa sababu za kufeli au kutokuwa na viwango na badala yake wakae na wazazi wao kwa lengo la kutafuta njia mbadala ili waweze kuwasaidia kuweza kufaulu.

Amesema imekuwa ni tabia kwa baadhi ya Walimu wa Skuli za Binafsi kuwafukuza watoto kwa madai ya kuweka rekodi mbaya za ufaulu katika Skuli zao jambo ambalo linawanyima fursa watoto katika kusoma.


 
Aidha amesema pia kuna baadhi ya Skuli hazifuati ratiba za Serikali za kufunga na kufungua Skuli hilo ni kosa kwa mujibu wa makubaliano yao, hivyo amewataka Skuli hizo kubadilika na kufuata makubaliano yao.

Hata hivyo amewataka kuhakikisha Skuli zao kudumisha mazingira ya usafi pamoja kuwahamasisha watoto kunawa mikono kwa sabuni ili kuweza kujikinga na maradhi mbalimbali ya kuambikiza yakiwemo ya UVIKO 19.

Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Elimu wamesema baadhi ya Skuli bado zimekuwa wagumu wa kulipa leseni za usajili hali ambayo inanyima fursa Wizara katika kuendeleza huduma zake za kielimu pamoja na wengine kutowapa mikataba Walimu wao na hivyo kuwakosesha huduma zao za msingi zikiwemo za ZSSF na nyengine.

Kuhusu suala la udhalilishaji Skuli za binafsi zinashindwa kuripoti matukio hayo sehemu inayohusika, na hata wanapofuatwa wanakuwa ni wagumu kutoa ushirikiano haki inayofanya kuendelea vitendo hivyo.


Akizungumzia sualala masomo, Mkurugenzi Taasisi ya Elimu mwalimu Suleiman Yahya Ame, amesema baadhi ya Skuli hazisomeshi kwa kufuata mitaala ya Elimu kama inavyoelekeza pamoja na baadhi ya walimu kutokuwa na ujuzi na viwango vya kufundishia kama taratibu zinavyoelekeza.

Pia amesema baadhi yao hawafuati Sera inavyoelekeza ya kutumia lugha ya kiswahili kwa kufundishia katika Skuli zao na hivyo kufundisha lugha ya kiengereza jambo ambalo utaratibu unavyoeleza.

Kuhusu kuwepo maktaba katika Skuli, Mkurugenzi wa Bodi ya Huduma za maktaba bi Sichana Haji Foum amesema kuna baadhi ya Skuli hasa za.binafsi zimekuwa na maktaba lkn wakutubi hamna na kama wapo hawana vigezo vya kuwepo ndani ya maktaba na hivyo kuwafanya Wanafunzi kukosa fursa nzuri ya kujisomea.

Pia amewataka Walimu hao kuwahamasisha Wanafunzi wao kusoma vitabu kwani itamsaidia mtoto kujenga uelewa zaidi na kuweza kufaulu vizuri katika masomo yao.

Wakitoa maoni yao katika mkutano huo baadhi ya walimu wakuu wa Skuli binafsi wamesema ni jambo zuri kufanya marekebisho ya mtaala lkn ni vyema kufanya utafiti kwa watoto kwa kuchambua vipaji vyao ili kuweza kutengeneza mitaala bora utakaowawezesha kuwasaidia watoto katika maisha yao.


 
Pia wameshauri juu ya suala zima la usajili wa Skuli za private kuwa kila baada ya miaka 4 au 5 badala ya kila mwaka kwani umekuwa ukiwapa usumbufu.

Aidha wameishukuru baraza la mitihani.kutoka na juhudi kubwa ya kidhibiti mitihani yao, laikini bado wana matatizo kutokana na matokeo wanayoyatoa kwani wamekuwa wakipata kesi za Wanafunzi kufaulu vizuri lkn anakuwa hajui kusoma, hivyo ameimba kubadilika kwa kuacha kuwapeleka wanafunzi mbele wasiokuwa na vigezo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post