Kikosi cha Yanga leo kimefungashiwa virago kwenye mashindano ya Kagame Cup 2021 baada ya kupoteza mbele ya Express FC ya Uganda.
Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-3 Express FC ambapo ni mabao ya Godfrey dk 14, Muzamiru dk 35 na Kambale dk 52 walipachika mabao kwa Express.
Bao pekee la Yanga limefungwa na Paul Godfrey dk 71 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 ambalo liliamsha nguvu kwa Wananchi lakini walishindwa kupata ushindi.
Kwa ushindi huo Express imeongoza kundi na Nafasi ya pili kushikwa na Big Bullets kutoka Malawi ambayo imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidhi ya Atlabara FC kutoka Sudan Kusin.
Post a Comment