Watu 24 wenye hasira wamewashambulia watumishi wa Ardhi toka kanda ya Mtwara na Morogoro pamoja na wa Wilaya ya Mlimba na kuchoma magari, pikipiki pamoja na vifaa vyao vingine, wakati wakiendelea na upimaji wa mashamba mkoani Morogoro.
Akizungumza Kamishina wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Morogoro Frank Mizikunte amesema kwamba watu hao wameunguza kifaa cha upimaji Chenye thamani ya zaidi ya Milion 60, Computer 3, Gari la Mkurugenzi, Pikipiki 3 za wasamamizi wa shamba .
Hata hivyo bado sababu za Watu hao kufanya uharibifu huo hazijajulikana .
Post a Comment