Wataalamu wa afya waeleza sababu za watoto kutoshambuliwa kwa kiasi kikubwa na Corona




Wataalamu wa tiba za binadamu wamesema kuwa kufa na kuzaliwa kwa cell mara kwa mara kwa watoto ndio sababu inayopelekea watoto kutoshambuliwa na Virusi vya UVIKO 19 vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya Mapafu.


Hayo yamebainishwa jijini Arusha na Mganga wa Hospitali ya Maunti Meru Dkt Sunday Wanyika wakati akitoa mada Kuhusu mlipuko wa Virusi vya UVIKO 19 kwenye mkutano wa wadau Kuhusu masuala ya msaada wa kisheria na upatikanaji haki kwa wananchi katika kipindi cha matumizi ya lugha ya kiswahili.



Mganga huyo ameeleza kuwa hali hiyo ndio imekuwa ikisababisha watoto kutoshambuliwa na Virusi hivyo maana vinapotaka kushambulia vinakuta cell zimekufa na kuanza kuzalishwa nyingine hivyo wao wakijikuta wanakuwa sugu na kuwa na uwezo wa kupokea na kuambukiza na kuathiri watu wazima.



"Zaidi ya aslimia 50 ya wagonjwa hawaonyeshi dalili na wanaongoza kwa kusambaza Virusi vya ugonjw huo hivyo wakati wa kujikinga usiwahofia ambao wameshaugua na kuonyesha dalili tu, muwe makini pia na kundi hilo, mpaka sasa watubmilioni 199 wameshapimwa na kukutw na maambukizi huku watu milioni 4 wakifariki na ugonjwa huo ulimwenguni,"amesema.



Ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanakuwa makini kwa kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo kwa kuchukua tahadhari zote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanachoma chanjo ambalo ni lazima kutokana na hali halisi ilivyo sasa, kutokwenda kwenye mikusanyiko isiyo ya lazima na kutulia majumbani, kuvaa barakoa ambazo zinakinga, kutumia vitakasa mikono na kunawa maji tiririka.



"Simu za mkononi zinaongoz kwa mambukizi kutokana n kushikwa mara kwa Mara nawasii wannachi muwe nazo makini kw kutumia vitakasa mikono mara kwa Mara,"amesisitiza.



Akizungumzia Virusi vya UVIKO 19 awamu ya sasa amesema viko tofauti sana na vile vya awamu ya kwanza vinasambaa kwa haraka zaidi na ni rahisi kusababisha kifo huku akitaja dalili namba moja kuwa ni kifua kuuma na kuwa kizito wakati awali ilikuwa ni kupta mfua, kukohoa na kushindwa kunusa.



Akifungua mkutano huo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Godfrey Mizengo Pinda amewataka mawakala wa sheria kwenye maeneo yao wapambanie afya za watu wao suala la chanjo ni muhimu Sana kwa maisha ya watanzania hivyo amewaasha washiriki wote wajitokeze kuchoma chanjo katika zoezi la uzinduzi wa chanjo litakalofanyika kesho jijini Arusha ili kujikinga.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post