Nimeangalia sana hili game la Bongo flavor Wasani wengine wanataka Kuwa Diamondplatnumz,
-Wanacopy kuanzia Life style
-Wanacopy Kuanzisha Record Label
-Wanacopy Kuongea na Kuvaa
-Wanacopy the way anavyoimba
-Kila msanii anataka nae awe na Maisha kama Diamondplatnumz
Bila kuangalia Diamondplatnumz amepambana 10 Years kuwa hapo na kupata Maendeleo aliyonayo
Unakuta msani ana miaka 3 or 5 anataka kumiliki kila kitu alichonacho Diamondplatnumz bila kuangalia diamondplatnumz alitokea wapi hadi kufika hapo
Ukiangalia Wasanii wengi wa bongo wanafanya vile vile kama diamondplatnumz hii inafanya tusione kitu kipya walichonacho bali tunaona Copy ya Diamondplatnumz
Wasanii wa Bongo Jitahidini Kila mtu awe na Identity Yake ili game la bongo flavor liwe tofauti na tupate mambo tofaut tofaut Sio lazima kila msani awekeze kwenye Record label au Media Vipo vitu vingi sana vya kuwekeza na vikakuingizia Mkwanja Mrefu tu tena kiulaini kuliko kuwekeza kwenye Record label au Media ambazo sina Stress na faida yake unaweza usione kwa haraka kwasababu ukimiliki Record label au Media Lazima uwekeze hela nyingi sana kuliko kupata faid
Wasani wa Marekani wangetaka kuwa kama Jay Z basi Na kumiliki Record label na Platform za kuuza Mziki basi Wasani wote Marekeni Wangekuwa na Record Label na Platform za kuuza mziki ila wengi Wameamua kuwa Na Identity zao na kuwekeza kwenye Biashara zingine Mfano kwenye NGUO, SHOES, PERFUME, HOTELS, RESTAURANT, ONLINE SHOPPING SHOPS, CLUBS, INDUSTRY na Wanaingiza Mikwanja Mirefu sana
My thought kwa Wasanii wa Bongo Flavor jaribuni kuwekeza kwenye vitu vipya ili Kuwa na Identity tofauti sio lazima kila msani amiliki Record Label au Media ebooo Wekezeni kwenye Vitu Vingine Vyenye Utofauti, Bongo now Record Label zimekuwa nyingi na Hazipati Faida kiivooo ni basi tu Waonekane kuna Record label zinasimamia Wasanii pia kuna Record label ambazo hazina faida yeyote kwa Wasanii wao unakuta msanii anatoa ngoma Deileee but hana Mafanikio Yeyote zaidi ya Kukik Instagram hata Hela ya Kupanga Ghetto hawana wanaishi kwenye HQ za Record Label zao this is Very Sad kama unaimba bila Faida yeyote na Mafanikio yeyote then Boss anavimba mjini. Kuwa Msanii mkubwa Mwenye Jina bila Mafanikio ni Uboya narudia tena Kuwa Msani mkubwa mwenye jina bila Mafanikio ni Uboya, Wazazi wanakuona Unatamba tu mjini ila hela ya kuwanunulia hata Sukari huna isee ni Matumizi mabaya ya kipaji chako.
Then Upcoming Wasanii angalieni Na Record Label za Kuwa Sign kuna Record Label zingine ni Jina tu ila Wasanii Wake wanakufa njaaa na hawana Mafanikio yeyote zaidi ya Kuunganishiwa WiFi na kukesha Instagram bila faida. ‘’SIO KILA KING’AACHO NI DHAHABU’’
Wasanii wa Bongo Flavor Pambaneni kuwa na Identity Yetu kuliko kupambana Kuwa Kama Diamondplatnumz cz inafanya game la bongo Flavor liwe na vitu vile vile tulivyovizoea ambavyo faida yake ni Ndogo.
Written by Granted Faith
Post a Comment