Wachina Wamuwekea Luis Bil 4.6 ni Baada ya Deal la Al Ahly Kubuma




WAKATI Al Ahly ikionekana kama kumpotezea kiungo mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone raia wa Msumbiji, inaelezwa timu ya Changchun Yatai FC ya nchini China, imeweka mezani kitita cha dola milioni mbili (zaidi ya Sh 4.6Bil za Kitanzania) ili kumnasa.


Imekuwa ikielezwa kuwa, Luis yuko mbioni kujiunga naAl Ahly kwa ofa ya dola 90000 (zaidi ya Sh 2Bil).


Dili la Luis na Al Ahly kwa sasa limesimamishwa baada ya klabu hiyo kukamilisha usajili wa Percy Tau raia wa Afrika Kusini aliyekuwa akicheza Brighton ya England.


Mmoja wa mawakala anayefanya kazi na Klabu ya Changchun Yatai, amelimabia Spoti Xtra kuwa, endapo Al Ahly wataamua kuachana na kiungo huyo, basi Luis atatua Changchun Yatai kwani wapo tayari kumsajili baada ya kuona uwezo wake kwenye mechi ya Simba na Yanga iliyochezwa Novemba 7, 2020 iliyomalizika kwa Yanga kushinda 1-0.


“Lengo la Wachina lilikuwa ni kumuona Michael Sarpong akiwa uwanjani, lakini baada ya kutumiwa video ya mechi ya Simba na Yanga, Ile ya Novemba 7, uwezo wa Luis Miquissone ulimvutia sana kocha na uongozi mzima wa Yatai.“


Wachina wanatambua kuwa kuna mazungumzo yalikuwa yakiendelea baina ya Simba na Al Ahly, ila baada ya kuona kuwa kuna winga kutoka Afrika Kusini amesajiliwa tayari, basi hilo limewapa nguvu ya kuleta mezani ofa yao.


“Bado haijawa kamili kama Ahly wameachana na Miquissone au la. Ila kwa sasa wanamvizia Miquissone.

Endapo tu Ahly wakiachana na kiungo huyo, wao wapo tayari kumnunua kwa dola milioni mbili. Hii ni mara mbili ya ofa aliyokuwa ameipata kule kwa Waarabu.”

STORI NA MANJIRO LYIMO, Dar es Salaama


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post