Roma amtolea uvivu Nikki Mbishi, Fanya muziki acha majungu badilika muda unaenda haurudi nyuma




Kupitia ukurasa wake wa Instagrama Roma Mkatoliki ameandika kuwa : “Niki!! Punguza Chuki, Chuki Zinakimaliza Kipaji Chako, Fanya Muziki Acha Makasiriko Kwa Wasanii Wenzako, Acha Chuki, Haikujengi Inakubomoa Kila Leo.



Kuna Wakati Unasingizia Hiyo Life Style Yako Hiyo Ndio HipHop, Big No, HipHop Sio Chuki, HipHop Ni Love & Peace. Utamaduni Wa HipHop Hautufundishi Chuki!! Unatufundisha UNIT’

Miaka Inakwenda Mzee Mwaka Wa 10 Huu Unatumia Same Approach Kwenye Game, Badilika, Watu Wamekua Sasa, Wanafocus Kwenye Majukumu Ya Familia,Wanalea Watoto, Wanaifanya Hii Game Biashara, Wana-Squash Beef Wana-Unit’ Keep Ya’ Head Up Son!!

Usirudishe Watu Kwenye Maisha Ambayo Washayapitia, Muda Hautoshi, Grow Up Mzee, Fanya Muziki Wako On Your Own Ways, Pasi Kuzungumzia Watu Wasiokuzungumzia Au Kukujibu, Ili Uje Ufurahie Matunda Ya Muziki Wako Kimpango, Tengeneza Content Ya Muziki Wako, Peleka Sokoni Ikipendwa Na Wengi Watanunua Simple Tu!! Shabiki Hahitaji Umshikie Gun Ndio Akupende, So Heshimu Na Wakumbatie Wachache Ulionao, Focus Kuwatengeneza Wengine Wengi!! Kumbuka Wengi Ni Mutual Fans So Zingatia Tu Contents Zako!!

Wakati Mwingine Unaowawekea Chuki, Wao Wanajitafuta Kwa Njia Zao Pasi Kuku-bother Wewe, Na Pengine Hata Wao Hawajafanikiwa Kiivo, Unawawekea Chuki Bure, Tabia Za Kichawi Hizo, Wakatoliki Hatufundishwi Hivo!! Badala Msapotiane Kuijenga Game Pamoja Kama Wenzenu, Nyie Mnataka Tuvutane Tuanguke Wote Then You Come Out Na Kujinadi You Are HIPHOP!! Bro This is 2021 Tumeshatoka Huko Kwenye Hizo Zama!!

Una Mu-Attack Kila Msanii, Una Matatizo Gani? Leo Huyu Hajui, Kesho Yule Anabebwa. Huheshimu Mkubwa Wala Mdogo, Unamchukia Hadi Mtoto Ambaye Hajazaliwa. Comon Man!! Thats Not HipHop!! Huwezi Kuwa Unajua Kila Kitu, Huwezi Kuwa Uko Sahihi Kila Kitu, Punguza U-Much Know!!


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post