#TAFAKATI-PRESS-Nimegundua Hapa kwetu Tanzania,Simba Sports club ndio club bora kwa sasa yenye uwezo mzuri katika medani ya kimataifa, club hii ina umri wa miaka 85 ,yenye takwimu haba za kisayansi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia.org ,Simba Sports Club ina jumla ya mashabiki 3 Million katika mtandao wake wa Instagram.
Alie kua Msemaji wa Simba ni Haji Manara, alie jua nini Yanga hawapendi kukisikia kuhusu Simba Sports Club, na nini Mashabiki wa Simba wanapenda kukusikia kuhusu tambo za Simba kisha anawadhihaki mashabiki wa Yanga, mashabiki wa Simba wanafurahia wakati Yanga wanachukia.
Mashabiki wa Yanga wanamchukia kisha wanamfuatilia sababu ni moja pekee, soka ni mchezo wa hisia, na Haji Manara alijua kucheza na hisia za mashabiki wa Yanga Na Simba kwa wakati mmoja.
Ametengeneza jina lililompa sifa, kiburi maringo, Haji Manara anasema anavyotaka na anataka anavyosema bila kufikiri wala kuwa na hofu yeyote, sababu amepata Endorsement na Simba wanampa pesa kwa kazi yake.
Haji Manara,anajiona yupo sahihi kwa kila anachosema na kuandika sababu alikua anapewa mshahara na Simba then,anapata Endorsement kwa ajili ya chake kinywa, Kinywa chake kinampa Pesa, ndio maana hatumii akili.
Ubora wa club ya Simba Sports Club, hawamuhitaji Haji Manara, katika kujenga Brand na kuongeza thamani ya Simba ,nje na ndani ya uwanja sababu Manara ni masikini wa :-
♧ Udadisi, "Curiosity Intelligence Quotient "
♧Hana staha njema
♧Uthabiti wa akili- Ufasaha wa Maarifa
♧Ujasiri wa akili
♧Heshima kwa jamii .
Majira haya Tanzania,imekuwa Incubator ya kuzalisha watu maarufu ambao ni Non Sense ,ndio maana hatutizami adabu,busara, weredi, nidhamu kwa watu tunaowapa Endorsement na ajira ndio maana tumepiga muhuri ujinga kuwa sehemu ya umaarufu.
Katika jamii yenye nidhamu na consciousness Haji Manara, alipaswa kuwajibishwa kwa kukosa hekima, busara, weredi na utimamu wa akili lakini Tanzania, Haji Manara ni maarufu sababu ya matumizi yake ya kinywa na sio akili.
NB
@bvrbvra anaiendesha @simbasctanzania kwa weledi na kanuni za mpira .Na sio kufata umaarufu wa mtu . @bvrbvra Huwezi kuchanganya BRAND kisha uchekewe hata siku moja . #TaalumaKwanza
Post a Comment