Muigizaji maarufu Jennifer Aniston aeleza kwanini amewatenga marafiki wasiotaka chanjo




Muigizaji maarufu Jennifer Aniston aeleza kwanini amewatenga marafiki wasiotaka chanjo

Jennifer Aniston amefafanua kwa nini amewatenga marafiki wake wengine ambao wamekataa chanjo.

Mapema wiki hii, mwigizaji huyo wa kipindi cha Friends alisema alikuwa "amepoteza watu wachache kutoka ratiba yake ya kila wiki" ambao walikuwa wameamua kukataa chanjo ya Covid.

Baadhi ya wafuasi wake wa Instagram wameuliza kwa nini alikuwa na wasiwasi sana, ikizingatiwa kwamba alikuwa amepata chanjo.

"Kwa sababu ikiwa una aina ya kirusi hicho, bado unaweza kuniambukiza ," aliandika Alhamisi.

"Ninaweza kuugua kidogo lakini sitalazwa hospitalini au kufa.

"Lakini naweza kumpa mtu mwingine ambaye hana chanjo na ambaye afya yake imeathirika (au ana maradhi nyemelezi) - na kwa hivyo ningeweka maisha yao hatarini."

Mwigizaji huyo alitoa maoni kwenye akaunti yake ya Instagram, ambayo inaruhusu watumiaji kutuma picha, video na ujumbe ambao unakaa tu kwa masaa 24.

Katika mahojiano yake na InStyle, yaliyochapishwa mnamo Jumanne, Aniston alisema: "Bado kuna kundi kubwa la watu ambao wanapinga-chanjo au hawasikilizi ukweli. Ni aibu ya kweli.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post