Campbell alisema ukaidi wa Zuma dhidi ya amri za mahakama na kifungo kimeigawa nchi.
Amesema ghasia zilizoanzishwa na watu wanaomuunga makono Zuma zilitishia maono ya baba wa taifa hilo hayati Nelson Mandela ya ustawi wa Afrika Kusini.
Mandela shujaa wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, aliongoza kipindi cha mabadiliko ya kutoka utawala wa watu weupe wachache katika miaka 1990, baada ya kifungo cha miaka 27 gerezani kwa sababu ya shughuli zake za kisiasa.
Jabu akijibu waraka huo alisema Campbell hana ‘’vigezo’’ ya kuzungumzia masuala ya Zuma.
Amesema baba yake alijitoa mno kwa ajili ya demokrasia ya Afrika Kusini.
"Unachokumbuka Afrika Kusini hakijawahi kuwa kielelezo cha Afrika Kusini ya kweli," Jabu aliandika akimaanisha urafiki wa Bi Campbell na Mandela.
Jabu alisema machafuko baada ya kifungo cha Zuma yalikuwa zaidi ya yanayomhusu baba yake.
Alisema raia wa Afrika Kusini walikuwa na njaa, hawana ajira na wamekuwa wakiulaumu utawala wa rais wa sasa Cyril Ramaphosa.
Post a Comment