Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya ya Arusha ASP Gwakisa Minga ameanza kutoa ushahidi wake katika kesi ya jinai 105/2021 inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjrao Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili kesi ambayo inanguruma katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha.
ASP GWAKISA anakuwa ni shahidi wa saba kwa upande wa mashtaka baada ya shahidi wa sita Bakari Msangi ushahidi wake kufungwa ikiwa umechukua siku sita kutokana na kuibuka mvutano wa hoja ya kuwasilishwa ama kutowasilishwa kwa nyaraka ya Maelezo alivyoandikisha Polisi kutumika kama Kielelezo Mahakamani hapo ikionekana kuchukua nafasi Kubwa zaidi wakati wa Ushahidi wake.
Katika Ushahidi wake ASP GWAKISA ameiambia Mahakama kwamba Siku ya Tarehe 09 Mwezi wa 02 Mwaka huu Majira ya Saa Nne za Usiku akiwa Kituoni alipokea Simu kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha KENNAN KIHONGOSI ambayo alimjuza kwamba aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ana Watuhumiwa na atawaleta Kituoni hapo hivyo awachunguze kama atabaini wana Shauri la Kijinai ampe mrejesho.
ASP Gwakisa ameaimabia mahakama kuwa Sabaya alipofika alimwambia kwamba amekamata Vijana Wawili wakiwa na Shauri la Uhujumu Uchumi kisha alifanya Mahojiano naye kama kuna sehemu vijana hao wameshtakiwa na tuhuma hizo lakini Sabaya alishindwa kuthibitisha.
Lengai ole Sabaya,Sylvester Nyegu,Daniel Bura kwa pamoja wanakabiliwa na mashataka Matatu yakiwemo ya Unyanganyi wa kutumia Silaha na Wizi wa Kutumia Silaha Makosa ambayo walikana kuyatenda.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi August 04 Mwaka huu na Watuhumiwa wamerudishwa rumande kutokana na Mashtaka yanayowakabili kutokuwa na dhamana.
Post a Comment