Meneja Afunguka "Nikikupa Nandy Humuwezi"

 


Meneja wa msanii Nandy Moko Biashara amesema kuna changamoto kubwa na ugumu kumsimamia msanii wa kike kwa sababu wana mambo mengi na amemtolea mfano Nandy kwa kusema akimpa mtu mwingine hawatawezana.

"Ugumu ni mkubwa sana, Nandy ni mmoja wa wasanii ambao nikikupa sasa hivi labda saa 1:20 basi saa 1:29 utanirudishia utasema humuwezi, kwa sababu ni mtoto wa kike 'make up' anatumia saa mbili, kuamka lazima mpigishane kelele lakini akiamka anakuwa active" 

Meneja Moko Biashara ameendelea kusema "Kitu kingine ni kwamba changamoto zake tayari nishazielewa itabidi tupambane tu, tunagombana, kuzimiana simu, wiki nzima hatusemeshani minuno tu lakini yote ni kujenga". 

Aidha Moko Biashara amesema kwa sasa ana muda wa miaka mitatu tangu aanze kufanya kazi na Nandy The African Princess



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post