Lionel Messi kuibukia Manchester City





BAADA ya taarifa rasmi  ku tolewa na Klabu ya Barcelona Agosti 4 zikieleza kuwa, nyota wao Lionel Messi raia wa Argentina anaondoka klabuni hapo baada ya kushindikana kusaini mkataba mpya kutokana na sheria ya matumizi ya fedha ya La Liga anatajwa kuingia kwenye anga za Manchester City.

Mtandao wa Barca umesema kuwa Klabu pamoja na Messi (34) mwenyewe wamefikia makubaliano hayo ya pamoja huku wakimshukuru kwa mchango wake mkubwa kwa klabu hiyo tangu ajiunge nayo akiwa mdogo na kumtakia maisha mema huko atakakokwenda.

Messi ambaye anashikilia taji la Ballon d'Or mara sita, alikuwa amekubali kuongeza kandarasi ya miaka mitano Barca huku akikubali pia mshahara wake kupunguzwa kwa asilimia 50 baada ya mkataba wake wa awali kumalizika June 30, mwaka huu.

Messi ametumia asilimia kubwa ya maisha yake ya soka akiwa Barca kuanzia kwenye academy kabla ya kupandishwa timu ya wakubawa mwaka 2003, amecheza michezo 672 na kufunga mabao 778.

Barcelona wamekuwa wakipitia maisha magumu ya kiuchumi kutokana na janga la Corona hali inayowalazimu kwa sasa kupunguza bajeti yao ya msimu ujao kuendana na sheria ya La Liga, pia wanapambana kuwapunguzia wachezaji wao mishahara ambao ni nahodha msaidizi Gerard Pique, Sergio Busquets na Sergi Roberto ambao wapo kwenye mazungumzo ya kupunguziwa asilimia 40 katika mikataba yao ijayo.

Pia wamejaribu kuwauza wachezaji wao kama Antoine Griezmann, Ousmane Dembele, Philippe Coutinho, Samuel Umtiti na Martin Braithwaite lakini hata wakifanya hivyo hali ni mbaya. Hivyo kwa sasa ni vita ya mabosi katika kuisaka saini ya nyota huyo.
 


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post