Ni muendelezo wa headlines za Kanye West kila uchwao, leo ameibuka na hili la kufanya onesho lingine tena katika uwanja wa Mercedes Benz mjini Atlanta, baada ya onesho la wiki iliyopita (listening party) ya album yake mpya #DONDA kupata mafanikio makubwa katika uwanja huo.
Onesho hilo maalum kwa ajili ya uzinduzi wa album hiyo limepangwa kufanyika usiku wa August 5, 2021 na tiketi zitaanza kuuzwa kuanzia Jumatatu, August 2. Bei ya Tiketi moja inaanzia ($30) hadi ($75) yaani TSh. 70,000 hadi 174,000/- Umeripoti mtandao wa Billboard. Usiku wa kuamkia leo Kanye ametujuza kupitia ukurasa wake wa instagram kwamba #DONDA itaachiwa rasmi usiku huo huo wa August 5.
Ye ambaye anaishi uwanjani hapo tangu Alhamis wiki iliyopita, ameandika ujumbe kwenye ubao, akisema: "Hii sio album bora ya mwaka, hii ni album ya maisha." - Kanye.
Post a Comment