Hakainde Hichilema mwenye umri wa miaka 59 sasa, ndiye rais mpya wa Zambia aliyetangazwa na tume ya uchaguzi nchini humo, akimuangusha rais aliyekuwepo madarakaki, Edgar Lungu.
alizaliwa huko Zambia wilaya ya Monze Juni 04, 1962 ni mfanyabiashara na mwanasiasa ambae sasa ni Rais mteule wa nchini Zambia!.
Ushindi huu wa Haikande aliyezaliwa Juni 04, 1962 katika Wilaya ya Monze nchini humo, unakuja mara baada ya ‘king’ang’anizi’ huyo kupoteza chaguzi tano dhidi ya chama tawala!
Hichilema, kiongozi wa chama cha upinzani cha United Party For National Development (UNDP) ambacho sasa ndicho kinakuwa chama tawala, hatimaye ameshinda nafasi ya urais kwa kura 2,810,75 dhidi ya mpinzani wake wa miaka mingi, Edgar Lungu wa kilichokuwa chama tawala cha Patriotic Front (PF).
Hili siyo jambo geni kwa Wazambia kufanya mabadiliko ya uongozi na kubadilisha vyama kupitia sanduku la kura, kwa takribani mara tatu viongozi waliokuwa madarakani waling’olewa na wapinzani.
Hichilema alichaguliwa kuwa Rais wa chama cha upinzani kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa chama hicho, Anderson Mazoka mwaka 2006. Pia aliwahi kutumikia wadhifa wa juu katika muungano wa vyama vitatu vya upinzani wa United Democratic Alliance (UDP).
Hichilema alishiriki uchaguzi wa kwanza wa urais kwa tiketi ya chama pinzani cha UNDP mwaka 2008 ambapo alishika nafasi ya tatu. Pia alikuwa ni kati ya wagombea wawili akishindwa kwa kura chache mwaka 2015 dhidi ya mpinzani wake, Edgar Lungu.
April, 2017 Hichilema alishikiliwa kwa tuhuma za kufanya jaribio la kuipindua serikali iliyokuwa madarakani na kufungwa miezi minne jela. Kifungo ambacho kwa Wazambia kilitafsiriwa kama jitihada za kuzima harakati za upinzani nchini humo.
Hichilema ni mume wa mke mmoja, Mutinta na baba wa watoto watatu, ukiachana na siasa king’anga’anizi huyu wa siasa ni mfanyabiashara mkubwa na tajiri nchini Zambia; duru zinaripoti kuwa Hichilema ni milionea na mmiliki wa biashara kubwa ya mifugo akishika nafasi ya pili nchini humo.
Huyu ndiyo Hichilema, rais tajiri Zambia aliyeshindwa chaguzi za urais kwa awamu tano!
Post a Comment