KIKOSI Cha Polisi cha Usalama Barabarani kimesema kuwa hakuna taarifa rasmi ya daladala kuwa idadi ya abiria kuendana na idadi viti (Level Seat.)
Askari akipata usumbufu wa Dereva kazi hiyo apewe aweze kuifanyia kazi kwani Mechi ngumu kazi kubwa ni kutoa Pasi ili mwingine aweze kucheza.
Akizungumza na Madereva na Abiria katika Kituo cha Daladala Mawasiliano Kamanda wa Polisi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni Notker Kilewa amesema kuwa taarifa hizo hutolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) au Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani na sio vinginevyo.
Amesema kuwa viongozi wa juu wakitangaza kinachofanyika ni utekelezaji wa agizo hilo kuwa na level seat.
Amesema kuwa Daladala mbovu hazitakiwi atakayekamatwa ni dereva pamoja na mmliki wa Daladala wote watawekwa ndani.
Kilewa amesema dereva wa daladala akirudisha Daladala mbovu kwa mmiliki, anajitokeza dereva mwingine kulitaka Daladala hiyo licha ya kuwa na ubovu akikamatwa dereva atawekwa ndani kazi ya mmiliki kuchukua Daladala yake na kufanya matengenezo.
Aidha amewataka Madereva na makondakta kuwa na ustaarabu wa kuvaa na kuoga kwani} makosa yaliyoanishwa juu ya mtu aliyemchafu kuchukuliwa hatua.
Kilewa amezitaka Daladala zote katika Mkoa huo kuwa na Jacks Mwanga sheria ambayo ilitungwa mwaka 2015 hivyo ni lazima itekelezwe.
Amewataka makondakta kuacha tabia ya kukimbilia Askari wa Usalama Barabarani pale anapokamatwa kwa kuwa ni ni kosa, Askari anawajibu wa kumfuata dereva wa gari na kusisitiza kuwa akiwakuta dereva na askari wote ndani.
- OPEN IN BROWSER
Post a Comment