Gomes Ashusha Mbadala wa Chama Simba SC





KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes ameagiza haraka aletewe kiungo mchezeshaji wa kati mwenye uwezo wa kutengeneza nafasi ‘asisti’ na kufunga mabao.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu ziwepo tetesi za nyota huyo kutimkia klabu ya Far Rabbat inayofundishwa na aliyekuwa kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck.

 

Rabbat ipo katika za mwisho za kukamilisha usajili wa Chama kwa dau la Sh 1.8Bil ambayo itamnunua baada ya kufikia muafaka mzuri.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Gomes alisema tayari ameuambia uongozi wa timu hiyo, anahitaji kiungo wa aina hiyo sambamba na mshambuliaji mmoja mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao.



Gomes alisema kuwa, kiungo na mshambuliaji huyo anaowahitaji ni lazima wawe wa kigeni na wenye uwezo na uzoefu wa mashindano ya kimataifa.

 

“Tayari tumekamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji katika kukiimarisha kikosi chetu kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.“

 

Tukiendelea na usajili wetu tayari nimeagiza nisajiliwe kiungo mmoja mchezeshaji wa kati wa aina ya Chama mwenye uwezo kufunga na kutengeneza nafasi,” alisema Gomes.

 

Usajili uliokamilika hadi wa sasa wa Simba ni winga Peter Banda (Malawi) na mshambuliaji Yusuph Mhilu huku wengine ambao wanatajwa kusaini lakini hawajatangazwa rasmi beki wa kati Inonga Baka Varane (DR Congo), Israel Patrick Mwenda (KMC), viungo washambuliaji Jimyson Mwanuke (Gwambina), Abdul Swamadu (Kagera Sugar), Kibu Dennis na kipa Jeremiah Kisubi (Prisons).

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post