Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Edith Mpinzile, amewaagiza wazazi, walimu na maafisa elimu kutoa elimu kwa wanafunzi kuwa chanjo ya Corona ni hiari na haitolewi kwao kufuatia vitendo vya wanafunzi kukimbia madarasani kila waonapo gari wakihofia kuchomwa chanjo hiyo.
Kwa mujibu wa Eatv.tv. Maagizo hayo amewayatoa wakati wa zoezi la uzinduzi wa chanjo wilayani humo uliozinduliwa na Mkuu wa wilaya kwenye kituo cha afya Katoro, ambapo amesisitiza kwamba elimu itolewe ili kuondoa hofu kwa watoto na watambue kwamba magari yanayofika mashuleni mwao yanaenda kwa shughuli maalum za ufuatiliaji wa elimu.
Baadhi ya wazazi waliofika kituoni hapo kwa ajili ya kupata chanjo wameelezea sababu zinazopelekea watoto kukimbia waonapo magari mashuleni mwao kwa kusema kwamba elimu wanayopewa na wazazi wao majumbani kwamba chanjo inagandisha damu zao ndiyo imewajengea watoto hao kuwa na hofu.
Chanjo ya corona inayotolewa sasa ya kampuni ya Johnson & Johnson hairuhusiwi kuchanjwa mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18 na zoezi lake linafanyika kwa hiari.
Post a Comment