Djigui atambulishwa rasmi Young Africans



Klabu ya Young Africans imethibitisha kumsajili Mlinda Lango kutoka nchini Mali Djigui Diarra.

Diara amethibitishwa kuwa mali halali ya ‘WANANCHI’ leo Jumapili (Agosti 08) mchana, baada ya kukamilisha mipango yote ya uhamisho wake akitokea Stade Malien ya nchini kwao Mali.

Kurasa za mitandao ya kijamii za Young Africans, zimeweka picha ya Video zikimuonesha Mlinda Lango huyo ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Mali kilichoshiriki Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika (CHAN).

Taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za klabu hiyo kongwe zimerembwa na kichwa cha habari kisemacho: “Djigui Diarra, sasa ni wa Manjano na Kijani…”

Usajili wa Djigui unamaanisha wazi huenda Young Africans ikaachana na Metacha Mnata ambaye mpaka sasa hajasaini mkataba mpya, huku akikabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post