Chama awatuliza Simba SC, “Msituchonganishe”

 


Kiungo fundi kutoka nchini Zambia na klabu ya Simba SC Clatous Chotta Chama, amewataka baadhi ya wadau wa soka Tanzania kuacha mpango wa kumgombanisha na Bosi wake Mohamed Dewji ‘Mo’.

Chama ametoa rai hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, kufuatia taharuki iliyojitokeza juzi Ijumaa (Agisti 06) alipokua Mubashara Kupitia mtandao huo.

Chama ameandika: “Jana (Juzi) ilikuwa kama drama ambayo hakuitarajia lakini sasa mambo yapo sawa.”

“Kama nilivyosema, mimi binafsi ninamthamini kila mtu anayeitakia mema Simba SC bila kupendelea au kushinikizwa.”

“Watu wengi wanapenda kutuona tukigombana bila sababu, wacha tusimpe adui sababu yoyote ya kutuangamiza!”

“Kuna vitu vya msingi kama Kutetea ubingwa wa Ligi Kuu na ASFC pia kufika mbali kwenye CAF Champions League.”

Wakati huo huo Chama amethibitisha taarifa za kuwa mbioni kurejea nchini baada ya mapumziko kuisha.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post