TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo Ijumaa, Agosti 20, 2021 imemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.
Hatua hiyo imekuja kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kutembelea miradi mbalimbali iliyopo katika Manispaa ya Temeke na kubaini kuwepo ubadhilifu wa fedha wakati wa utekelezaji wa miradi hiyooo.
Post a Comment