Bill Gates kuachana na mkewe baada ya miaka 27 ya ndoa


Mwanzilishi wa Microsoft, bilionea wa Marekani Bill Gates na mkewe Melinda Gates wameamua kuachana.

Bill Gates alitangaza kuhusu uamuzi wa kupeana talaka na mke wake kwenye akaunti yake ya Twitter, kwa kuandika,

"Baada ya kufikiria sana juu ya uhusiano wetu, tumefanya uamuzi wa kuipa mwisho ndoa yetu".

Read More: Nafasi 6 za Ajira Startimes Zilizotangazwa Leo

Aliendelea kwa kusema kwamba yeye na mkewa walilea watoto 3 wakati wa miaka yao 27 ya ndoa, walisaidia watu kote ulimwenguni kuishi maisha yenye afya na tija kwa msingi waliouanzisha, na jambo hili ltaendelea.

"Lakini hatufikiri tunaweza kukua pamoja kama wenzi katika hatua inayofuata ya maisha yetu." aliongeza.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post