Aliyesema “Shahidi Yangu Mungu” Aibua Mazito Mahakamani




Ushahidi wa kesi ya jinai inayomkabili mchungaji Merchades Mugishagwe na mkewe Agripina Maganja, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Bukoba umefungwa leo, baada ya shahidi namba tatu kwa upande wa washtakiwa aliyetajwa kuwa ni Mungu kutofika mahakamani hapo.

 

Utetezi wa kesi ya jinai namba 35 ya mwaka 2021 ilifunguliwa February 2, mwaka huu. Mugishagwe na mkewe wanatuhumiwa kukataa kuwapeleka watoto wao shule kwa madai ya kuwa kufanya hivyo ni dhambi kwa maana maandiko ya Mungu hayaruhusu watoto kwenda shule.

 

Familia hiyo inao watoto watano na wote walikuwa hawasomi na mkubwa kati yao ni wa kike mwenye umri wa miaka 13, mbali na kutokwenda shule, wakiwa wadogo hawajawahi kupelekwa kliniki na pia wakiumwa hawapelekwi hospitali.

 

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro, alimwagiza afisa elimu ya msingi wa manispaa hiyo, kuwakamata na kuwapeleka shuleni kwa nguvu watoto watatu wa familia hiyo huku wazazi wao wakishtakiwa.

 

Mchungaji Buberwa wa Kanisa la Wakristo washikao amri za Mungu, ambalo makao yake makuu yako mbinguni, alisema hayuko tayari kuruhusu watoto wake kutenda dhambi kwa kwenda shule, huku mkewe Agripina Maganja, akimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa Mungu atasimama kuwatetea.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post