Zari, Mondi Wajifungia Bafuni





WAHENGA walipata kusema; ‘wagombanapo wapenzi, shika jembe ukalime!’ Ndicho anachosisitiza mmoja wa mameneja wa staa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul au Diamond Platnumz, Sallam Sharif maarufu kama Sallam SK.


Hayo yalijiri baada ya kukumbwa na mkasa mkubwa wakati penzi la Diamond au Mondi na mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady ’ lilipokuwa limekolea. Sallam anaaminiwa kuwa na ubuyu mwingi kumhusu msanii huyo anayetikisa Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla.

 

MKASA ULIKUWA HIVI
Akisimulia mkasa ambao ulimpa wakati mgumu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Sallam anasema kuwa, tukio hilo lilitokea wakati Mondi akishuti video ya ngoma yake iliyokwenda kwa jina la Utanipenda.

 

Anasema kuwa, katika tukio hilo, Mondi akiwa na timu yake kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), alikwenda kushuti video hiyo Afrika Kusini ambapo pia ni makazi ya mwanamama Zari mwenye pesa zake.

 

KUMBE WALIJIFUNGIA BAFUNI
Anasema kuwa, wakati wakiendelea kushuti video hiyo iliyokuwa ikisimamiwa na direkta ajulikanaye kwa jina la The God Father, walishtuka kutomuona Mondi eneo la tukio na walipokuja kutahamaki, kumbe alikuwa amejifungia bafuni na Zari.

 

“Tulipomgongea Mondi atoke ili aje kushuti scene yake, akatoka kisha akaniambia nenda kajieleze kwa shemeji yako, analia huko…anasema wewe umemwambia kuwa mimi bado ninampenda Wema.

 

“Nilishtuka kidogo, kwa sababu sijawahi kukaa kuzungumzia uhusiano wao na yeyote kati yao, baada ya kumweleza ukweli kuhusu msimamo wangu, lakini pia nikakumbuka Zari alikuwa tayari amepiga vyombo kidogo, hivyo nikahisi alikuwa anambipu Mondi kujua thamani ya upendo wake kwake,” anasema.

 

Hata hivyo, kazi ya kushuti iliendelea vizuri kwa sababu bahati nzuri, Zari tayari alikuwa amekishacheza kipande chake.

 

Alisema kuwa, Mondi alimalizia kipande chake na kuendelea na mambo mengine.Aidha, Sallam alisisitiza kuwa yeye anafanya kazi na Mondi na siyo Nasibu Abdul, hapa akimaanisha kuwa anafanya kazi na msanii au staa na siyo mtu binafsi ambaye anaweza kuingilia uhuru wake na familia yake hivyo kamwe heshima yake hataishusha kwa Mondi kwa kuingilia masuala yake binafsi.

 

SI MARA YA KWANZA KUVUJISHA UBUYU
Hata hivyo, si mara ya kwanza kwa Sallam kuanika ubuyu kuhusu mapito ya msanii huyo, kwa Juni, mwaka huu, wakati Mondi alipokwenda Afrika Kusini, Sallam alitupia picha za Mondi na Zari wakiwa kimahaba, kiasi cha wengi kuhisi wawili hao wamerudiana.

 

Sallam alitupia picha hizo kwenye mtandao wake wa Instagram zinazoonesha Mondi amemshika kiuno Zari huku mkono mwingine ukiwa mabegani, lakini kubwa zaidi wakiwa wamevaa saresare.

 

ZARI NA MONDI KUTEMANA
Ikumbukwe kuwa ukweli kuhusu Zari na Mondi kutemana ulidhihirika Februari 14, 2018 baada ya Zari kuposti ua jeusi ambalo limepata umaarufu miongoni mwa mastaa wa kibongo kama ishara ya wapendanao kutengana.

TORI: MWANDISHI WETU, DAR




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post