Wanaodai Katiba Mpya Walikimbia Bunge la Katiba





MBUNGE wa Ngega Vijijini, Dkt. Hamisi ameamua kuvunja ukimya na kufunguka kuhusu baadhi ya wanasiasa wanaodai mchakato wa katiba mpya uanze ili kuliwezesha Taifa kupata Katiba inayoendana na mahitaji ya wananchi kwa sasa.

 

Kupitia mtandao wa Twitter, Kigwangalla amesema; Chama cha siasa huanzishwa kuwaleta pamoja watu wenye mawazo na sera zenye kufanana. Lengo kuu ni kuleta ustawi wa watu. CCM haikuahidi mchakato wa Katiba kwenye ilani, bali ustawi wa watu. Nakubaliana na Mhe. Rais, kwa sasa tukomae na ustawi wa uchumi, Katiba baadaye!

 

Kwa kuzingatia Katiba yetu ilipotoka, na uwepo wa mabadiliko makubwa ya mwaka 1984, na jinsi ilivyoweza kutuvusha kwenye kipindi kigumu cha msiba mzito kwa amani, na ilivyoweza kudumisha Muungano wetu kwa kipindi chote hiki, mabadiliko ya Katiba yanaweza kusubiri kidogo kwanza.

 

Wanaodai Katiba Mpya leo ndiyo waliokimbia Bunge la Katiba. Walikimbia kitu gani na je walichokimbia kimeondoka ama kipo? Kama kipo, wana uhakika gani kwamba safari hii kitabadilika? Ama ni ajenda ya kisiasa tu kuwayumbisha wananchi na kujaribu kuchelewesha shughuli za maendeleo?

 

Kama Katiba tuliyonayo imetuwezesha kuvuka kipindi kigumu cha msiba, na imetuwezesha kujenga barabara na kufikisha maji ya Ziwa Victoria Tabora, inafaa kuendelea nayo kwa muda mpaka hapo mahitaji ya kweli ya Katiba Mpya yatakapojitokeza. Tusikubali kutoka kwenye reli!

 

Kama Katiba tuliyonayo imeweza kutusaidia kufika hapa tulipo, tusiwe na pupa wala haraka kuibadili. Kukiwa na uhitaji wa kweli, na wala siyo uhitaji wa wanasiasa wachache wenye maslahi binafsi ya kisiasa!

 

Kuna watu wanadai kuwa Katiba Mpya inahitajika sasa hivi, sijui wameambiwa na wananchi wa wapi, maana mimi sijawahi kudaiwa na wananchi wenzangu wa Nzega Vijijini ninaowawakilisha. Wao wananidai umeme, maji, barabara na shule. Kwa sasa tujikite na haya kwanza, Katiba baadaye.

 

Wanasiasa wanaanzisha mjadala wa Katiba Mpya kukidhi matakwa ya kisiasa ya kwao binafsi na siyo hitajio la msingi la wananchi walio wengi. Katiba Mpya haiweki ugali mezani, wala dawa zahanati, inaweza kusubiri. CHADEMA watafute ajenda ya maendeleo ya watu, na siyo Katiba Mpya!

 

Tafuteni ajenda mpya ya kutokea. Muacheni Rais wetu mpya ahangaike na ustawi wetu wananchi. Tusimshinikize na Hoja inayoweza kusubiri. Kwani hao CHADEMA wamepata wapi ‘uamuzi wa wananchi’ kuwa tunataka Katiba Mpya?

 

Wakati wa wananchi kudai Katiba Mpya haujafika. Hivyo, hii si ajenda ya wananchi ya ‘kufa na kupona’, ni ajenda ya wanasiasa, tena wachache. Madai ya sasa ni ya CHADEMA. Katiba tuliyonayo haijashindwa kutatua changamoto zetu, imeweza kutupa amani, mshkamano na ustawi wa kiuchumi.

 

Maneno ya kusingiziwa hayawezi kukukosesha usingizi. Unahitaji muda tu kabla ukweli haujadhihiri na kushinda. Nasimamia principles za ukweli, uwazi na integrity kwenye siasa zangu. Hizi ni assets zisizochoka. Mark this tweet. Fuatilia Hoja nilizosimamia utaelewa ninachosema!

 

Nimemsikia Mzee wangu Jaji Werema. Kama issue yake ni hilo moja tu la ‘Madaraka makubwa ya Rais’, angeweza kushauri ‘marekebisho’ ya Katiba tu (kwenye eneo hilo) na siyo ‘Katiba Mpya’ kabisa!

 

Katiba ya Marekani imerekebishwa mara 27, na imedumu toka Mwaka 1789, zaidi ya miaka 230, na bado Kuna kero na changamoto kwenye maisha ya watu. Majirani zetu kadhaa wameandika katiba mpya na bado kuna kero/changamoto na wengine wanajuta kubadili Katiba zao. Katiba isubiri!

 

Tunaohangaika na biashara mtaani ni mashahidi jinsi hela ilivyokuwa ngumu, jinsi ambavyo watu wana madeni na hawawezi kuyalipa. Sisi tunapenda Rais wetu ashughulikie hii liquidity crisis, atie chachu kukua Kwa uchumi na siyo kuhangaika na siasa za Katiba Mpya ama Hoja za CHADEMA!

 

Katiba tuliyonayo ni Bora sana. Hata kama ina mapungufu, basi madogo madogo sana. Na hayo yanaweza kusubiri kwa Kweli. Mzee Kikwete alisikia kilio cha wadai Katiba Mpya akaanzisha mchakato ili kuyarekebisha, kwa nia njema kabisa; lakini wale wale waliokuwa wanadai walikimbia!

 

Mwalimu Mabala, CCM hatukuvuruga mchakato, bali CHADEMA walisusia mchakato baada ya kuona Hoja yao ya kuvunja Muungano haipiti! Kwenye kikao siyo lazima Hoja yako ipite. Unapaswa usikilizwe lakini ujue tu walio wengi watashinda! Ndiyo demokrasia hiyo.

 

Kuna tofauti kati ya ku-amend na kuandika upya. Mimi nadhani kama Kuna haja ya amendment hapa na pale wanaweza kujenga hoja hiyo inaweza kushawishi, na siyo jambo la kufa na kupona. Ama la haraka kiasi hicho. Linaweza kusubiri. Lakini siyo kuibeza hii tuliyonayo.

 

Katiba ya Marekani ya Mwaka 1789 iliandika ‘all men are created equal’ lakini bado Rais wa Kwanza wa Marekani na wenzake 11 waliofuatia waliMILIKI watumwa! Katiba inaweza kuweka ‘statement’ nzuri sana na kusiwe na utekelezaji. Kwa kuwa hii inatoa haki, usawa na amani, tuiheshimu.

 

Katiba ya Marekani ya Mwaka 1789 iliandika ‘all men are created equal’ lakini bado miaka 180 baadaye bi. Rosa Park alitakiwa kumpisha kiti dume la kizungu! Katiba inaweza kuweka ‘statement’ nzuri, bila utekelezaji ni kazi bure.Kwa kuwa hii inatoa haki, usawa na amani, tuiheshimu.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post