Wanachama 17 NHIF Mbeya mbaroni

Mbeya. Wanachama 17 wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) mkoani Mbeya wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh188 milioni.

Wanadaiwa kuchukua dawa nyingi kwenye vituo vya afya na kuziuza kwenye hospitali binafsi na maduka ya dawa.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Julai 6, 2021 na mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera katika mkutano wake na waandishi wa habari baada kupokea taarifa ya ripoti ya   upotevu wa fedha  kutoka kwa naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin  Mollel.

Amesema mbali na wanachama hao kushikiliwa na polisi,  pia vituo saba vya afya vimebainika kufanyika  wizi wa dawa za Sh1.6 bilioni na kwamba uongozi wa mkoa huo kwa kushirikiana na wizara ya afya wametoa muda wahusika kurejesha fedha hizo.

"Ripoti inaeleza wizi umetokana na utoaji  wa dawa kwa wanachama  waliokuwa wakienda kupata huduma na kupewa dawa kwa wingi na kisha kwenda kuuza,



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post