Waliowahi Kufanya Kazi za Ndani Saudi Arabia Wadai Walikuwa Watumwa


Wasichana waliowahi kwenda kufanya kazi za ndani nchini Saudi Arabia wakitokea #Kenya wamesema wanakuwa watumwa na hunyimwa Haki zao za Msingi za Binadamu

Madalali na Mawakala wamedaiwa kuingia mikataba ambayo haijulikani na wafanyakazi hao, hali inayoleta sintofahamu kwakuwa wao hupokea ujira mdogo

Mateso wanayopata ni pamoja na kupigwa kikatili na kunyimwa Huduma za Afya ikielezwa, wakiumwa huishia kupewa Panadol na kutakiwa kuendelea na kazi


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post