Walichosema Miss Tanzania baada ya msimamo wa Basata

 


Dar es Salaam. Baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kutengua maamuzi ya kamati ya Miss Tanzania kumuengua Miss Tanzania 202/2021, Rosey Manfere kuwa mwakilishi wa nchi katika mashindano ya urembo ya dunia, kamati hiyo yajibu mapigo.

Jana Basata ilitoa msimamo wa kuendelea kumtambua mrembo huyo baada ya kamati ya maandalizi ya Miss Tanzania kumuengua na kumpa nafasi hiyo mshindi wa pili, Juliana Rugamisa.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, Basata iliitisha kikao  cha kukutanisha pande zote mbili yaani Miss Tanzania, Rose na kamati ya maandalizi lakini wajumbe wa kamati hiyo hawakutokea kwa kile walichoeleza kutingwa na majukumu mengine.

Licha ya kutotokea kwa wawakilishi wa kamati hiyo, kikao kilifanyika kwa kumsikiliza Miss aliyekuwa ameongozana na mwanasheria wake na mwisho wa kikao maamuzi yaliyoafikiwa ni kutengua uamuzi ya kamati hiyo na kuagiza, jina la Rosey kupelekwa kwenye  mashindano ya Miss World.

Hata hivyo saa chache baada ya kutolewa kwa uamuzi huo, kupitia ukurasa wao wa Miss Tanzania, waliandika

 “Mashindano ya Miss Tanzania yanaendeshwa kwa sheria taratibu na kanuni .Tunawasihi warembo mnaotafuta nafasi adimu ya kuwa warembo wa Taifa mzingatie sheria na kanuni.

“Maelekezo ya kamati ambayo mengi ni ya kukuongoza wewe kuilinda heshima yako na taji, ukizingua maana yake utazinguana na wahusika na sheria itachukua mkondo wake.

Andiko hilo liliendelea kuelezwa kuwa, 

“utaelekezwa ukikaidi hatutasita kumpa mshindi wa pili kwa mujibu wa kanuni na sheria zetu.

“Kwa kifupi kama unamakucha yafiche hadi urudi Miss World vinginevyo hakutakua na wa kumlaumu. Ukimlaumu aliyechukua nafasi yako wakati alikupongeza wakati wewe unashinda utakua ni ubinafsi.

Sheria imempa nafasi ni haki yake, ushauri wa bure kwa warembo wa Tanzania.

Ukiachilia mbali andiko hilo, bado wanaendelea kupiga kampeni ya kumtangaza Juliana kama mwakilishi kwa kuweka picha zake na kuonyesha shughuli mbalimbali za kijamii ambazo anaendelea nazo.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post