Bodi ya Ligi Tanzania bara TPLB imetangaza waamuzi watakao chezesha mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Simba SC dhidi ya Yanga SC mchezo utakao chezwa siku ya Jumamosi Julai 3, 2021, uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam.
Emmanuel Mwandembwa kutoka Arusha ndio atakaye kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo huo wa kiporo mchezo namba 208 wa VPL utakaoanza kutimua vumbi Saa 11:00 Jioni, ambapo atasaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Frank Komba wa Dar es salaam, mwamuzi msaidizi namba mbili Hamdan Said wa Mtwara na mwamuzi namba nne ni Ramadhani Kayoko wa Dar es salaam.
Hii hapa orodha kamili ya maofisa watakao simamia mchezo huo wa watani wa jadi wa soka la Tanznaia Simba na Yanga.
Post a Comment