Moyo wa mwanamke unahitaji mwanaume mnyenyekevu mwenye huruma na mapenzi ya dhati. Mwanaume atakae mbembeleza wakati wa huzuni. Mwanaume atakaeguswa na changamoto zake hata kwa hali kama hana mali.
Mwanaume makini hasiti kumuhudumia mke wake kwasababu anajua kutoa ni baraka na ndio kitu kinachompa utulivu wa dhati mwanamke. Mwanamke haitaji hela tu bali nae anahitaji mapenzi ya dhati na ukaribu wa mwanaume.
Usafi sio jukumu la mwanamke pekee hata mwanaume anatakiwa kujiandaa vyema mbele ya mkewe muda wote awapo mbele yake. Kauli chafu na kebehi sio ndio uwanaume bali ni ujinga na ulimbukeni. Acha kumtukana mkeo.
Mwanamke hakuolewa ili aje kuwa mtumwa ndani ya nyumba bali lengo la ndoa ni ibada lakini ni msingi wa furaha wa moyo na mwili. Mke si mali ya familia yako bali mke ni msaidizi wako hivyo basi usikubali ndugu kumtesa mke wako nawe ukiwepo.
Mwanaume anatakiwa kuwa mtatuzi wa matatizo na sio chanzo cha matatizo. Ni aibu mwanaume kuwa na gubu ndani ya nyumba yake. Kila afanyalo mwanamke kwake baya na halina thamani tabia hii kamwe haiwezi kumea kwa mwanaume makini. Mwanamke nae ni mtu, hivyo anahitaji kuthaminiwa na kuenziwa. Mpe heshima mkeo.
Post a Comment