Maandamano yenye ghasia yameendelea nchini Afrika Kusini usiku kucha na Jumatatu asubuhi juu ya kufungwa jela kwa rais wa zamani Jacob Zuma. Duka moja kubwa huko Pietermaritzburg, katika mkoa wa KwaZulu-Natal lilichomwa moto Jumatatu asubuhi wakati uporaji na uharibifu wa mali ukiendelea Jumatatu asubuhi.
Picha za jengo hilo likiteketea moto na usumbufu uliosababishwa na maandamano hayo zimesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii: Makumi ya watu wamekamatwa na barabara zimefungwa wakati vikosi vya usalama vikishughulikia vurugu zinazoendelea.
Maandamano hayo yanaendelea huku mahakama ya kikatiba ikisikiza rufaa ya Zuma dhidi ya kifungo chake kwa kukaidi agizo la mahakama. Korti inafanya tathmini ya uamuzi wake wa hapo awali na huenda ikatoa maagizo baadaye ikiwa hukumu hiyo itatekelezwa.
Afrika Kusini imepeleka jeshi kukabiliana na ghasia zilizotokea baada ya kufungwa kwa rais wa zamani wa taifa hilo Jacob Zuma. Maduka yalivamiwa na majengo yalichomwa moto siku ya Jumatatu, wakati Zuma akisikiliza kesi yake katika mahakama ya juu.
Watu wapatao sita wameuawa na 200 kukamatwa tangu ghasia hizo zianze wiki iliyopita. Zuma amehukumiwa kwa kosa la kuidharau mahakama baada ya kushindwa kuhudhuria kesi yake ya madai ya rushwa wakati wa utawala wake.
Zuma mwenye umri wa miaka 79, ambaye alikanusha kuhusika katika madai ya rushwa, lakini alienda mwenyewe polisi wiki iliyopita ili kuanza kfungo chake cha miezi 15.
Akiwa anatarajia kifungo chake kupunguzwa katika mahakama ya katiba. Hata hivyo wataalamu wa sheria wanasema nafasi ya kushinda ni ndogo sana. Kesi hiyo imeibua matukio ambayo hayakutarajiwa nchini humo ambapo hawajawahi kushuhudia kuona rais wa zamani akifungwa gerezani.
Jumatatu ,picha za video zilionesha maduka makubwa yakichomwa moto katika mji wa Pietermaritzburg, katika eneo alikotokea Zuma, KwaZulu-Natal, na watu wakifanya maandamano. Ghasia zilienea mpaka Johannesburg, katika jimbo la Gauteng.
Jumapil , waandamanaji walionekana wakiandamana katika maeneo ya biashara ya mjini Johannesburg. Jeshi limesema limeagizwa kwenda kusaidia kupunguza ghasia ambazo zimekuwa zikiendelea kwa siku kadhaa. Rais Cyril Ramaphosa amesisitiza utulivu , akisema hakuna maelezo juu ya vurugu hizo.
Zuma alikamatwa kawa kukaidi maelezo ya kutoa ushaidi juu ya kesi ya rushwa ilyokuwa inamkabili wakati yuko madarakani. Alihudhuria mara moja tu kwenye uchunguzi wa kile kilichojulikana kama madai ya kuporwa kwa mali za serikali.
Post a Comment