Baada ya kupata mafanikio makubwa Jijini Atlanta, Wakazi wa New York wanaweza nao kuishuhudia listening party ya Kanye West, kwa mujibu wa ukurasa wa Deux ambao unadili na habari za mastaa, umeripoti kwamba Kanye tayari amekodi ukumbi wa Madison Square Garden kwa ajili ya kufanya sehemu ya pili ya usikilizaji wa album yake mpya, DONDA.
Taarifa zinaeleza kwamba usiku huo Kanye West atafanya uzinduzi wa bidhaa zake za mavazi 'YEEZY GAP' chini ya ushirikiano na Kampuni ya GAP. Usiku huo pia inaweza kuachiwa album yake mpya ambayo imetajwa kutoka Agosti 6, mara baada ya kuahirishwa wiki iliyopita.
Kumbukumbu zinaeleza, Kanye atafanya kama alichokifanya mwaka 2016 pale alipoachia album yake #TheLifeOfPablo kwenye uzinduzi wa Yeezy Season 3 katika ukumbi huo huo wa Madison Square Garden
Post a Comment