Baadhi ya mashabiki amekuwa wakiwalinganisha au kuwashindanisha Nandy na Zuchu kutokana wote wanafanya vizuri kimuziki, hata hivyo kuna tofauti kati yao;
1. Tangu ametoka kimuziki Nandy hajawahi kuwa chini ya lebo zaidi kunolewa na Tanzania House of Talent (THT). Hata hivyo, Zuchu ametolewa kimuziki na lebo ya WCB Wasafi yake Diamond Platnumz.
2. Kabla ya kutoka Nandy alifanya vizuri katika shindano la Tecno Own The Stage nchini Nigeria aliposhika nafasi ya pili na kuzawadiwa Tsh. Milioni 36. Wakati Zuchu hajawahi kutamba katika mashindano ya kusaka vipaji.
3. Nandy tayari ana albam, The African Princess iliyotoka Novemba 2018 na Extended Playlist (EP) mbili, Zuchu hana albamu ila ametoa EPl moja, I Am Zuchu iliyotoka Aprili 2020.
4. Hadi sasa Nandy ameshinda tuzo zaidi ya tatu kubwa ambazo ni All Africa Music Awards (AFRIMA) 2017, Maranatha Awards 2018 na African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) 2020, huku Zuchu akiwa na tuzo moja, AFRIMMA 2020.
5. Nandy Instagram ana followers Milioni 5.2, Facebook Milioni 1.6 na YouTube 823,000. Kwa upande wa Zuchu, Instagram Milioni 3, Facebook Milioni 1.1 na YouTube Milioni 1.4.
6. Nandy ana kolabo nyingi za kimataifa kuliko Zuchu, The African Princess huyo ameshirikiana na wasanii kama Willy Paul, Joeboy na Koffie Olomide. Zuchu ana kolabo moja tu aliyofanya na Joeboy.
7. Nje wa muziki @officialnandy ametengeneza himaya ya biashara kuliko Zuchu. Nandy ni mmiliki wa kampuni ya Nandy Bridal inayotoa huduma kwa maharusi, pia ana Nandy Festival. @officialzuchu hana kampuni bali ni balozi wa kampuni mbalimbali akitangazia bidhaa za nywele, vipodozi n.k.
8. Nandy ni mkali wa melodi katika uimbaji lakini sio uandishi na ndio sababu nyimbo zake nyingi ameandikiwa. Zuchu anaandika sana kutokana hicho ni moja ya vigezo hadi kusainiwa WCB Wasafi.
9. Nandy hatokei familia ya muziki kama ilivyo kwa Zuchu ambaye mama yake mzazi, Malkia wa Taarab nchini, Khadija Kopa tayari ametengeneza himaya yake kwenye muziki kwa miaka mingi.
10. Tayari Nandy amefanya show nyingi na kubwa za kimataifa kuliko Zuchu. Nandy ameweza kufanya tour kwenye nchi kama Kenya, Marekani…
Post a Comment