Ujenzi wa sanamu la Magufuli viwanja vya sabasaba



Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TANTRADE imesaini hati ya makubaliano yenye jumla ya shilingi milioni 420 ya ujenzi wa sanamu la Hayati John Pombe Magafuli, na ukarabati wa kumbi kubwa za kisasa kwenye maonyesho ya sabasaba ya 45.

Wakati wa utiaji saini wa hati hiyo Baina ya TANTRADE na NBC Benki, Mkurugenzi wa TANTRAdE Rutageruka Sabi amesma kuwa, ujenzi wa sanamu la Hayati Magufuli linalenga kuenzi kumbukumbu, jitihada na mchango wa JPM katika kuinua uchumi wa viwanda

Amesema kuwa uchumi wa viwanda ni kichocheo kikubwa cha biashara nchini na ndio msingi hata wa maonyesho ya sabasaba ambayo kwa mwaka huu ni maonyesho ya 45.

Akielezea Mkataba huo Mkurugenzi Sabi amesema ni mkataba unaohusisha kipindi cha miaka mitatu huku akitaja maeneo mengine yatakayoguswa na ufadhili huo ni pamoja na ukarabati wa kumbi mbalimbali ikiwemo ukumbi mkumbwa unaofahamika kama SabaSaba wenye ukubwa wa mita za mraba 1,600, ambapo ndipo yanapofanyika maonyesho ya madini.


 
Sambamba na hayo sabi amesema ni heshima kwa benki hiyo kuingia katika ushirikiano huo kwa kuwa utatoa fursa kwa kufanikisha azma ya msingi ya kuendeleza kuwahudumia wadau wake wakiwemo wafanyabiashara wanaoshiriki maonesho hayo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post