Tetesi za soka kimataifa





Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba ananyatiwa na Paris St-Germain msimu huu wa joto na klabu hiyo ya Ligue 1 inapanga kuuwauza wachezaji kadhaa kukusanya £50m wanazoamini zitafanikisha azma ya kumpata Pogba. (Mirror)
United hawajapokea mawasiliano yoyote kutoka kwa PSG kuhusu uwezekanao wa uhamisho wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliye na umri wa maika 28. (Manchester Evening News)

Barcelona wanajikakamua kuuza wachezaji ili kufadhili mkataba wa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, kabla ya msimu mpya kuanza. (Guardian)

Mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, 28, ana matumaini uhamisho wake kwenda Manchester United utakamilishwa siku chache zijazo. (AS - in Spanish)

Ajenti wa kiungo wa kati wa Juventus Mtaliano Nicolo Fagioli, 20 - ambaye ni sehemu ya mkataba wa kubadilishana mchezaji wa Sassuolo Manuel Locatelli - amethibitisha kuwa mahasimu wao Arsenal wamewasilisha dau la £34m kumnunua. (Sky Italy, via London Evening Standard)

Arsenal wako tayari kuipatia Leicester City wachezaji kadhaa - akiwemo winga Muingereza Reiss Nelson, 21 - kama sehemu ya mkataba wa kumsaini kiungo wa kati wa England James Maddison, 24. (Daily Mail)

Gunners wameimarisha juhudi za kumsaka kipa wa Barcelona Mbrazil Neto, 31. (Mundo Deportivo, via The Sun)

Chelsea huenda wakawasilisha dau la £135m kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20. (ESPN, via 90 min)

Tottenham wanakaribia kufikia makubaliano na winga wa Sevilla Mhispania Bryan Gil ambao utamwezesha mshambuliaji wa Argentina Erik Lamela kuhamia klabu hiyo ya La Liga club. (Sky Sports)

Manchester United wana nafasi ya kuwasajili wachezaji wakuu wawili kabla ya dirisha la uhamisho wa wachezaji kufungwa ndadi ya wiki sita. Beki wa Atletico Madrid na England Kieran Trippier ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa. (Manchester Evening News)

Juventus wanatathmini uwezekano wa mkataba wa kubadilishana wachezaji ambao utamwezesha Cristiano Ronaldo, 36, kujiunga na PSG nao wampate tena mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 28. (L'Equipe via Daily Star)

Juventus wameweka £35m kuwa bei ya kumuulizia mlinzi wa Mturuki Merih Demiral, ambaye anahusishwa na uhamisho wa kwenda Everton. (Goal)

Leeds United wanapigiwa upatu kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Muingereza Lewis Bate,18. (Daily Mail)

Winga wa Bayer Leverkusen Demarai Gray,25, alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu siku ya Jumanne anapokaribia kusajiliwa na Everton. (Sky Sports)

Chelsea wanamtaka kipa wa zamani wa Fulham Marcus Bettinelli, 29, kujiunga nao msimu ujao. (The Telegraph)




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post