Stamina Afunguka Kuhusu Madai ya Uchawa wa Shetta


Stamina Shorwebwenzi amesema Shetta ni mtu ambaye anaangalia sana fursa na kwa vitu anavyofanya hawezi kumuweka kwenye engo ya uchawa kama baadhi ya watu wanavyomtafsiri.


"Shetta ni mjanja mjanja sana, kati ya wamba ambao nawaaminia yeye kiboko anajua kuitafuta fursa na haiachi ule ndio unyama na inavyotakiwa, watu wengi wanaeka kwenye angle ya uchawa kwangu mimi simuoni kama ni uchawa namuona kama fighter" ameeleza Stamina 


Stamina ameongeza kusema kuna vitu vingine anavyovifanya Shetta ambavyo yeye hawezi kuvifanya kwa sababu kwenye maisha lazima kuwe na mtu ambaye anachangamka.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post