HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa wanaamini kwamba kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga watapata pointi tatu muhimu ili watangazwe kuwa mabingwa.
Ikiwa ipo nafasi ya kwanza na pointi 73 inahitaji pointi tatu ili kufikisha pointi 76 ambazo hazitafikiwa na watani wao wa jadi walio nafasi ya pili na pointi 67 ndani ya ligi.
Manara amesema kuwa maandalizi ya mchezo yapo kamili hivyo wataingia uwanjani wachezaji kwa nidhamu na wakitambua kwamba utakuwa mchezo mgumu huku hesabu zao ikiwa ni kupata pointi tatu ili watangazwe kuwa mabingwa.
"Mechi itakuwa ngumu hilo lipo wazi na tunawaheshimu wapinzani wetu lakini ni lazima tupate pointi tatu ili tutangazwe kuwa mabingwa.
"Niwaombe mashabiki wajitokeze kwa wingi na mara baada ya mchezo tuwapigie makofi wachezaji kwa wingi kwa kuweza kutwaa ubingwa wa ligi mara nne mfululizo," .
Post a Comment