Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara imefikia tamati hii leo kwa michezo tisa kupigwa katika viwanja tofauti, huku katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam mabingwa mara nne mfululizo klabu ya Simba wamepata ushindi wa magaoli 4 kwa 0 dhidi ya Namungo .
Mabao ya Simba yamefungwa na washambuliaji wake Medie Kagere, Chris Mugalu aliyefunga mara mbili na John Bocco akifunga moja.
Simba imemaliza msimu ikiwa na alama zake 83 wakati waliokuwa wapinzani wao wa karibu Yanga ambao jioni ya leo wametoka suluhu na Dodoma Jiji huko katika dimba la Jamhuri, wamemaliza katika nafasi ya pili wakiwa na alama 74.
Washindi wa tatu Azam Fc wameshinda bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ,shukrani kwa nyota wake Mudathir Yahya na wamemaliza msimu wakiwa na alama 64.
Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa leo katika kumaliza msimu wa ligi kuu Tanzania bara 2021/22 ni;
Ruvu shooting 0 – 1 Azam FC
Mbeya City 4 – 0 Biashara United
KMC FC 1 – 0 IHEFU FC
JKT Tanzania 2 – 1 Mtibwa Sugar
Tanzania Prisons 1 – 1 Gwambina FC
Polisi Tanzania 1 – 0 Mwadui FC
Coastal Union 3 – 1 Kagera Sugar
Kwa matokeo haya sasa Coastal Union na Mtibwa Sugar watakwenda kucheza mtoano kugombea kusalia ligi kuu, Huku timu za JKT Tanzania, Gwambina FC, Ihefu FC na Mwadui FC wao wameshuka daraja moja kwa moja.
Post a Comment