Simba Wafunguka "Tulicheza Vibaya Mbele ya Yanga"

 


 KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa kipindi cha kwanza walicheza vibaya mbele ya Yanga jambo ambalo lilifanya wakafungwa mapema.

Julai 3 itabaki kwenye rekodi ya Gomes pamoja na Simba kiujumla kwa kupoteza mchezo wao wa ligi mbele ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.


Gomes amesema kuwa walishindwa kucheza vizuri kipindi cha kwanza na walicheza vibaya jambo lililowafanya washindwe kupata ushindi.


"Ninasikitika kupoteza mchezo mbele ya wapinzani wangu Yanga kwani sikutarajia kuona matokeo ya aina hiyo kwa wachezaji wangu pamoja na timu kiujumla.


"Ila kwa kuwa tumepoteza hakuna namna tutajipanga kwa ajili ya mechi zijazo ila ukweli ni kwamba ninastahili lawama zote mimi ninazibeba licha ya kwamba wachezaji walicheza vibaya.


"Kipindi cha kwanza ambapo tulifungwa mapema tulicheza vibaya na wachezaji wangu walitengeneza nafasi walishindwa kuzitumia hivyo ninasikitika kweli," amesema.


Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya kwanza ina pointi 73 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili ina pointi 70.


Yanga imecheza jumla ya mechi 32 huku Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 30 inasaka pointi tatu ili kuweza kutimiza lengo la kuwa mabingwa wa ligi mara ya nne mfululizo.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post