"Sijawahi Kuwa na Msimamo Tofauti Kuhusu Corona" Waziri Gwajima




Waziri wa afya wa Tanzania Dorothy Gwajima amesema kwamba msimamo wake kuhusu janga la corona haujawahi kubadilika .

Hii ni baada ya waziri huyo kupokea shutuma hasa mitandaoni kwamba awali katika utawala uliopita alikuwa na msimamo tofauti na wa sasa kuhusu hatari ya virusi hivyo na sasa anaonekana kuunga mkono juhudi za rais Samia Suluhu kutumia mbinu zinazotumiwa na nchi nyingine kupambana na janga hilo.

Gwajima amesema matumizi ya nyungu ni tiba ya asili ambayo iliwasaidia wengi na bado itatumika lakini sasa panafaa kuwa na tahadhari zaidi kwasababu ya aina mbalimbali ya virusi vya Corona


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post