Shahidi kesi ya Sabaya awatambua watuhumiwa asema mmoja hayupo mahakamani




Shahidi wa sita katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, Bakari Msangi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa katika gwaride la utambuzi polisi aliweza kuwatambua watu wawili akiwemo mmoja wa vijana waliokuwa wanatekeleza amri ya Sabaya ya kuwapiga.

Shahidi huyo ambaye ni Diwani wa CCM Kata ya Sombetini amemaliza kutoa ushahidi wake leo Alhamisi Julai 29, 2021 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo na anatarajia kuanza kuhojiwa na jopo la mawakili sita wa utetezi.


Shahidi huyo akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka alidai kuwatambua Daniel Bura (mshitakiwa wa tatu) na Deogratias Peter ambapo alidai alimtambua Bura baada ya kumsikia Sabaya akimtaja kwa jina katika duka la Shaahid Store.


Kuhusu Peter alidai kumkariri kwani ndiye aliyekuwa anatekeleza amri ya Sabaya ya kuwapiga ila anashangaa kutokumuona mahakamani hapo na washitakiwa wengine.


Alipotakiwa na Wakili Kweka kuangalia mahakamani hapo na kuieleza mahakama kama aliowatambua wako hapo alionyesha mshitakiwa wa tatu huku akishangaa kutokumuona Peter wakati alimtambua polisi.


"Niliitwa kwenye gwaride la utambuzi ambapo nilimtambua Daniel na Peter ila nashangaa Peter simuoni hapa mahakamani na ndiye alikuwa akitekeleza amri ya Jenerali Sabaya ya kupiga w


Awali alidai mahakamani hapo kuwa alipoenda kuandika maelezo yake katika Kituo cha Polisi Kati, mpelelezi wa shauri lake aliyemtaja kwa jina moja la Kaleb (aliyedai ni marehemu kwa sasa), alikataa kumsomea maelezo hayo kabla hajasaini na kumwambia ni kinyume na taratibu za sheria za polisi.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post