Serikali mpya ya Israel imepata pigo kubwa la kwanza Bungeni leo baada ya kushindwa kurefusha sheria yenye utata inayowazuia Wapalestina ambao wameolewa na Waisraeli na wanaishi katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza, kupewa kibali cha ukaazi au Uraia wa Israel.
Baada ya kura kupigwa Bungeni kila upande ulipata kura 59 na kuufanya huu kuwa mtihani wa kwanza wa kisiasa kwa Waziri Mkuu mpya Naftali Bennett mwezi mmoja tangu achukue madaraka kuiongoza Serikali ya muungano inayojumuisha vyama vya mrengo wa kushoto, kati na vyama vya kiarabu pamoja na chama chake cha kizalendo.
Israel ilipitisha sheria hiyo mwaka 2003 wakati wa maandamano ya Wapalestina ikisema Wapalestina walioolewa na Waisraeli walitumia nafasi hiyo ya kisheria kusaidia katika mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya Israel.
Waziri mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu anayeiita Serikali ya Bennett kuwa kitisho kwa usalama wa Israel alipiga kura ya kupinga urefushaji wa sheria hiyo.
Post a Comment