Sakata la Mwanamuziki Zuchu Kumloga Dada wa Mondi Qeen Darleen




KWA mara ya kwanza, msanii mpya kunako Bongo Fleva, Zuhura Othaman au Zuchu amefunguka juu ya stori za mitandaoni kwamba, anamloga msanii mwenzake ndani ya Wasafi, Mwanahawa Abdul almaarufu Queen Darleen.

Zuchu amefunguka kuhusu hilo jana, visiwani hapa, alipokuwa akitangaza ujio wa tamasha lake la Zuchu Home Coming Concert ambalo litafanyika Jumamosi ya Agosti 21, mwaka huu.

“Hatuna tatizo lolote, mimi na dada Darleen tunaongea sana, tunapigiana simu tunacheka na vitu vingine vinaendelea. “Ukichukua kila kitu kinachosemwa utagombana na kila mtu na tasnia yetu ni ndogo, unaweza ukajikuta huongei na watu wote.“Na kuonesha kwamba, maisha yanaendelea, hata yeye Darleen atakuwepo kwenye tamasha langu,” anasema Zuchu.

Tamasha lake hilo litafanyika visiwani Zanzibar ambapo Zuchu ametoa kipaumbele kwa wasanii wa Zanzibar na aina zote za muziki wa Zanzibar kupewa nafasi kwenye tamasha hilo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post