Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Silivester Nyegu na Daniel Mbula, leo wamepandishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha baada ya kesi yao kuhamishwa kutoka Mahakama ya Mkoa wa Arusha.
Kutokana na ufinyu wa nafasi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, kesi hiyo imepelekwa kusikilizwa katika vyumba vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ambapo inatarajiwa kusikilizwa kwa siku 14 mfululizo.
Post a Comment