Mwimbaji Ray C ameonyesha kuchoshwa na kauli mbalimbali anazozitoa #Mwijaku kuhusiana na Bongo Fleva.
Kupitia ukurasa wake wa instagram, Ray C amepost video clip ya msanii Ruby akiimba, huku akiuliza; "Nani kasema Tanzania hakuna vipaji?
RayC amempa za uso Mwijaku akieleza kuwa, kile anachosema ni kutulisha matango mchana kweupee.
"Nani kasema Tanzania hakuna vipaji? Y’all!!!! when it comes to Bongo Flava I speak my mind I don’t give a damn!! coz Bongo Flava iko damuni na nitaipenda na kuitetea daima mana ndio muziki ninaousikiliza miaka yote hata kama siko Bongo!!!
Sema nini!!! Mwijaku unatulisha matango mchana kweupeeee 🙄🙄🙄 kama mnawaza Grammy basi itakuwa ndoto kama wasemaji na wainuaji wa vipaji wa sasa ni Mwijaku... Rest in Peace Ruge Mutahaba.
Unamsikitisha sana huko aliko maana umetokea mikononi mwake na unaujua muziki vizuri sema unaleta ukatuni!It is showbiz right!? Poa basi Fanya ziara ya studio mbaliimbali hapo Tanzania kama kweli una nia ya kuinua vipaji vya ukweli maana vimejaa mitaani huko najua wajua na nyumbani kwako THT kuna watoto walioachwa njia panda baada ya bosi kuondoka na unajua kabisa wana vipaji vya kuzaliwa wanahitaji kusikika kupitia hiyohiyo media ambayo aliekufanya uwepo hapo hayupo leo.
Najua kwako kutrend ni fahari ila unawakosea sana vijana wenye vipaji vya ukweli..Unajitoa akili kutulisha mpunga wakati ndani ya nafsi yako unajua unapuyanga. Unatulisha matango...
Post a Comment