Rais Samia Akutana na Mkurugenzi wa Barrick Gold





Rais Samia Suluhu Hassan, leo Julai 7, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Barrick Gold, Mark Bristow, Ikulu jijini Dodoma na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa kampuni hiyo pamoja na Kampuni ya Twiga.

 

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Jaffar Haniu, katika mazungumzo hayo, Bristow amemhakikishia Rais Samia kuwa Barrick itaendelea kushirikiana na serikali katika uwekezaji wa sekta ya madini nchini na kwamba wapo tayari kuendelea kuwekeza katika maeneo mengi zaidi.

 

Kwa upande wake, Rais Samia amemhakikishia mwekezaji huyo kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao kwa kutekeleza makubaliano yote yanayofikiwa, kwa lengo la kuhakikisha madini yanazinufaisha pande zote mbili kwa manufaa ya taifa.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post