Rais Samia Suluhu Hassan, leo Julai 5, 2021 amemteua Bi Fatma Ayoub Mwinyimvua Simba kuwa Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, kabla ya uteuzi huo, Bi Fatma alikuwa mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMS) jijini Dar es Salaam na kwamba uteuzi huo umeanza leo.
Post a Comment